Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema atahakikisha anasaidia kupata vyanzo vya fedha vya kuaminika ili kuhakikisha safari na ushiriki wa michezo mingi zaidi katika Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Mhe Nape Nnauye

Waziri Nape Nnauye ameyazungumza hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokutana na wadau wa michezo nchini kupanga mikakati ya ushiriki wa soka kwenye mashindano ambapo ameutaka ushiriki wa serikali katika kusaidia soka nchini ikiwa ni pamoja na kufanya mchezo huo kuwa jambo la nchi ili kuukuza na kutangaza zaidi.

“Olimpiki tunaenda kama Watanzania na siyo kama timu pekee hivyo tunatakiwa tushikamane pamoja na kuhakikisha tunashinda pamoja, na ninaposema tunatakiwa kufanya soka kuwa jambo la nchi namaanisha kuwa itasaidia ili hata watu waliokabidhiwa dhamana wakubali kujisahihisha pale wanapokosea, ” amesema Waziri huyo.

Nape amewataka pia wadau wa soka na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuiunga mkono Serengeti Boys katika mashindano ya Afrika nchini Gabon ili ifanye vizuri na kuwa kama sehemu ya mtaji wa kwenda Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.
Katika kuhakikisha Serengeti Boys inafanya vizuri, Waziri Nape ametangaza kamati ya watu 10 wakiwemo wasanii Diamond na Alikiba pamoja na waandishi wa habari za michezo na wadau wengine

Advertisements

EWURA IMETANGAZA BEI ELEKEZI ZA MAFUTA ya PETROLI NA DIZELI 

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei elekezi za mafuta ya petroli na dizeli kwa mwezi Machi mwaka huu ambapo mafuta ya petroli na disel kwa bei za jumla na reja reja imepanda.

Kituo cha mauzo ya mafuta

Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Ewura Bw. Titus Kaguo amesema bei hizo zimepanda kutokana na mabadiliko katika soko la dunia ambapo kwa upande wa mafuta ya rejareja, petroli imepanda kwa wastani wa Shilingi 102 kwa lita sawa na asilimia 5.18 huku dizeli ikiwa imepanda kwa shilingi 51 kwa lita sawa na ongezeko la asilimia 2.76.

Bw. Kaguo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi Leo Machi 01, na zitabadilika kulingana na nguvu ya soko katika mkoa husika ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, lita moja ya petroli itauzwa kwa shilingi 2,060 na dizeli Shilingi 1,913 huku kukiwa hakuna mabadiliko yoyote ya bei kwa upande wa mafuta ya taa

NAPE AJITOSA RASMI SAFARI YA TOKYO NA GABONI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema atahakikisha anasaidia kupata vyanzo vya fedha vya kuaminika ili kuhakikisha safari na ushiriki wa michezo mingi zaidi katika Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo, Mhe Nape Nnauye

Waziri Nape Nnauye ameyazungumza hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokutana na wadau wa michezo nchini kupanga mikakati ya ushiriki wa soka kwenye mashindano ambapo ameutaka ushiriki wa serikali katika kusaidia soka nchini ikiwa ni pamoja na kufanya mchezo huo kuwa jambo la nchi ili kuukuza na kutangaza zaidi.

“Olimpiki tunaenda kama Watanzania na siyo kama timu pekee hivyo tunatakiwa tushikamane pamoja na kuhakikisha tunashinda pamoja, na ninaposema tunatakiwa kufanya soka kuwa jambo la nchi namaanisha kuwa itasaidia ili hata watu waliokabidhiwa dhamana wakubali kujisahihisha pale wanapokosea, ” amesema Waziri huyo.

Nape amewataka pia wadau wa soka na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kuiunga mkono Serengeti Boys katika mashindano ya Afrika nchini Gabon ili ifanye vizuri na kuwa kama sehemu ya mtaji wa kwenda Olimpiki 2020 jijini Tokyo, nchini Japan inafanikiwa.

Katika kuhakikisha Serengeti Boys inafanya vizuri, Waziri Nape ametangaza kamati ya watu 10 wakiwemo wasanii Diamond na Alikiba pamoja na waandishi wa habari za michezo na wadau wengine

SERIKALI YAISHUKURU AFDB KUKUBALI KUFADHILI MIRADI YA UJENZI WA BARABARA NA USAFIRISHAJI WA UMEME ILI KUFUNGUA KANDA YA MAGHARIBI

Waziri wa Fedha na Mipango ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa kukubali kuendelea kufadhili miradi ya maendeleo ya kipaumbele hususani ya ujenzi wa barabara na usafirishaji wa umeme ili kufungua fursa za kiuchumi katika kanda ya Magharibi.

Dkt. Mpango ametoa shukrani hizo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaowakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) ameiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo kuanza mapema iwezekanavyo.

Amesema kuwa Benki hiyo iliahidi kutoa fedha ili kujenga barabara ya Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na kwamba mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo na Nchi jirani ya Burundi.

Pia mradi wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi huu utawezesha Mikoa ya ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa Viwanda vidogo na vya kati.

“Katika kikao hicho tumewaeleza Wakurugenzi hao wa AfDB hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua katika kutatua changamoto ya Miundombinu ya Umeme na Barabara, kupanua fursa za Ajira, na kuharakisha maendeleo ya ukuaji wa Sekta ya Kilimo ambayo inategemewa na wananchi wengi” Alifafanua Waziri Mpango.

 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb), akiongoza mkutano ulio wakutanisha Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu hali ya uchumi wa Tanzania huku ahadi zilizotolewa na Benki hiyo zikijadiliwa katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kulia)na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Doto James (kushoto) wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani) alipokuwa akielezea umuhimu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) wakati akizungumza na Wakurugenzi 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki hiyo Mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam. 

 Maafisa waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa Makini Maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (hayupo) pichani wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini anayeiwakilisha nchi hiyo (AfDB) Bi. Elizabeth Mmakgoshilekethe (kulia) akiipongeza Serikali kwa kuweka vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na vile vya Benki ya Maendeleo ya Afrika katika Mkutano na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mpango (Mb) katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es Salaam.

tanzaniayetu