Category Archives: Siasa

MBUNGE ATAKA KUTUMIA KISWAHILI UCHAGUZI EALA 

Baadhi ya wabunge wameibua hoja ya kutaka Kiswahili kitumike kuwauliza maswali wagombea wa Chadema wanaojinadi kuwania nafasi ya ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala). 
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ baada ya kupewa ruhusa na Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kwa kuwa sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge nchini ni kujua kusoma na kuandika, hivyo Kiswahili kitumike kuwauliza maswali.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililla amesema mbunge anaweza kuuliza swali kwa Kiswahili lakini mgombea atapaswa kujibu wa Kiingereza.

Baada ya jibu hilo, Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema iwapo swali litaulizwa kwa Kiswahili, basi atafutwe wa kutafsiri kwa kuwa hata majibu hayo hatayaelewa.

Advertisements

UJUMBE WA PROFESSOR JAY KWA WANANCHI WA MIKUMI KUPITIA SOCIAL NETWORK 

 April 19, 2017 Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Professor Jay’ ameutumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha ujumbe kwa watu wa jimbo lake kuelekea kwenye Bunge linaloedelea mjini Dodoma akiwaomba ushauri kuelekea majibu ya swali kuhusu kero ya maji.

“Mikumi Stand up…

Leo tunakwenda kupata majibu ya swali letu namba 75 kuhusu Kero kubwa ya MAJI jimboni Mikumi! ! Kuna ushauri wowote wa nyongeza kuhusu kero ya maji jimboni Mikumi? ? Naomba maoni yako ili tuongeze kwenye swali la nyongeza” – Professor Jay.

MASHABIKI WA VYAMA VYA SIASA IFAKARA WALITAKA KUVAMIA KITUO CHA KUPIGIA KURA MBASA MLIMANI

Ifakara. Polisi wilayani Ifakara  wamelazimika kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki wa vyama vya siasa waliotaka kuvamia kituo cha kupigia kura cha Mbasa Mlimani.
Mashabiki hao walitaka kuvamia kituo hicho katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mbasa, baada ya mawakala kutokubaliana na matokeo.  

Katika vurugu hizo askari Huruma Mkisi alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe kichwani na mtu asiyefahamika na hivyo kupelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis ya Ifakara kwa ajili ya matibabu. 

Awali, mashabiki hao walianza kwa kulalamikia matokeo ya uchaguzi kucheleweshwa kutangazwa na hivyo kuwatilia shaka mawakala ambao walikuwa wakibishana kuhusu idadi ya kura walizopata wagombea wao. 
Akitangaza matokeo, msimamizi wa Uchaguzi huo Gaston Kaputa alimtaja mshindi  wa nafasi ya mwenyekiti wa Kijiji cha Kisawila kuwa ni Shaaban Salahange wa CCM  aliyepata kura 557 aliyefuatiwa na Odric Matimbwa (Chadema) aliyepata kura 528 huku mgombea wa NCCR-Mageuzi Bakari Mkungundile akiambulia kura mbili.

MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE MKOANI PWANI RIDHIWAN KIKWETE AMEFUNGUKA BAADA YA MAMA YAKE JANA KUTEULIWA KUWA MBUNGE.

Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete amefunguka baada ya mama yake jana kuteuliwa na Rais Magufili kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ridhiwan Kikwete amesema kuwa mama Salma Kikwete ni mwanamke wa shoka kwani amewezesha wasichana wengi nchini Tanzania kupata elimu na amekuwa mtetezi wa haki za wanawake hivyo anaamini kupata nafasi ya kuwa Mbunge itakwenda kuwezesha mapambano kuwa sheria rasmi. 

“Umekuwa mtetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu. Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera sana kwa uteuzi‬. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena” aliandika Mhe. Ridhiwan Kikwete

UWOYA AWAJIA JUU WASANII WANAODAI KULIPWA NA CCM WAKATI WA KAMPENI 

Msanii Irene Uwoya amekerwa na kitendo cha wasanii wenzake kutumia vyombo vya habari vibaya kwa kutangaza kuwa walilipwa pesa zao za kampeni kipindi cha uchaguzi mwaka 2015 na kuacha kufanya mambo yenye tija ndani ya jamii.

 

                               Irene Uwoya

Uwo- ya ameandika katika ukurasa wake ya instagram kuwa kitendo hicho ni kujishushia heshima na kutaka vitu vingine vibaki kwa wanaohusika tu sio lazima kuongea kila kitu maana watu wanatamani muda mwingine kusikia vitu ambavyo wanahisi vina faida na sio kila saa kuongelea mambo ya chama.

“Kuna vitu vinaboa sana, kweli kada mzima wa CCM unasimama hadharani unasema tulilipwa kufanya ‘campaign’ ?, hata kama lakini unafundisha nini jamiii?. Unafundisha jamiii kwamba yote tuliyoongea kuhusu CCM hatukuyamanisha ni kwasababu tulilipwa? unaiambia jamiii ulikuwa mnawadanganya sababu mlilipwa?”. Ameandika Irene Uwoya

Aidha msanii huyo amewashauri wenzake wajifunze kunyamaza muda mwingine kama hakuna ulazima wa kuongea maana wanaweza kuhisi wanajenga kumbe ndiyo wanaharibu kabisa.

“Embu tufanye kazi zinazotuhusu jamanii, ‘Nigeria’ wenzetu sasa wako ‘Hollywood’ wanaigiza huko sisi hata ‘Nigeria’ kwenyewe bado hatuja pasua”. Ameandika kwa kusisitiza msanii huyo

Irene amewasisitizia wasanii wenzake waache kushabikia ujinga na vitu visivyokuwa na msaada kwa jamiii na kuwataka wapige kazi ili waweze kutoboa ndani ya tasnia yao  vinginevyo wataishia kuiona ‘Hollywood’ katika televisheni.

Huu ndiyo ujumbe wake…