Category Archives: Muziki

DIAMOND AMUANDIKIA UJUMBE RAY C KUPITIA UKURASA WAKE WA INSTAGRAM 

​Ikiwa ni siku chache baada ya Mwimbaji Ray C kuachia wimbo wake wa Unanimaliza, Leo Msanii wa BongoFleva, Diamond Platnumz kupitia account yake ya Instagram ameandika ujumbe huu…..
Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….
Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….
niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku

Advertisements

MAMBO MATANO ALIYO YASEMA RAY KIGOSI YA DIAMOND NA MAREHEMU KANUMBA KUAMBIWA NI MA FREEMASON 

Muigizaji staa wa Bongo movie Ray Kigosi ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopata mafanikio makubwa kwenye industry ya filamu nchini na kufanikiwa kujijengea jina na heshima kwa jamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray ametoa ujumbe ambao unalenga kutoa uelewa kwa mashabiki hasa wa filamu na muziki nchini ambao wamekuwa wakiwahusisha baadhi ya mastaa wanaofanya vizuri na imani tofauti.
Katika kuufikisha ujumbe huo Ray amewatolea mfano staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz na muigizaji nyota Stiven Kanumba aliyefariki miaka mitano iliyopita ambaye alifanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie.
Ray Kigosi ameandika…
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!
2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!
3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.

Anadai alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO

Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.
5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.
Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.

DIAMOND PLATNUMZ KUFANYA KOLABO NA YOUNG KILLER


​Stori inayotrend kwa sasa katika social networks ni kuhusu Diamond Platnumz ambaye ni kiongozi wa WCB kuzindua brand yake ya ‘manukato’ yaitwayo Chibu Perfume ambayo imepokelewa vizuri na mashabiki wake.

Mbali na uzinduzi huo wa Chibu Perfume, jana April 24 2017 kupitia XXL ya Clouds FM staa huyo wa Marry You ametoa tathmini ya Bongo fleva akisema kuwa umekuwa na ushindani mkubwa akidai umewashinda hata Wanigeria kwa sasa.

Aidha, Diamond amegusia kuhusu kufanya collabo na rapa Young Killer akisema amefanya naye kazi kwa lengo la kunyanyua muziki wa nyumbani kwa sababu kufanya kazi tena na Wanaigeria hakuwashtui watu kama zamani:“Kitu ambacho watu hawakifahamu, ukifanya kazi na Wanigeria watu hawashtuki kabisa. Nimefanya collabo na Young Killer kunyanyua muziki. Muziki wetu umekuwa wa kiushindani kabisa, lazima tujitume. Wanigeria now hawapo juu yetu, muziki wetu upo juu sasa.” – Diamond Platnumz.

JOH MAKINI AJIVUNIA KUFANANISHWA N JAY Z

Joh Makini amesema ufananisho huo uko wazi kwa kuwa kiwango cha muziki wake ni mkubwa kiasi ambacho watu wanaomzunguka na wapenzi wa kazi zake hawaoni mtu mwingine wa kumfananishia naye isipokuwa msanii huyo kutoka Ughaibuni.

Jay Z ni ‘role model’ wangu…mimi naimba maisha ya sinoni daraja mbili na Tanzania na Jay Z anaimba maisha ya Brooklyn na Marekani, nafikiri nipo katika ‘level’ ambayo hawaoni mtu mwingine wa kunifananisha naye…Kwahiyo mimi naona poa kwa sababu kama unanifananisha na Jay z ‘yeah i like it’ kuliko ungenifananisha na mtu mwingine”. Alisema Joh Makini

Kwa upande mwingine msanii huyo amedai changamoto na vikwazo anavyokutana navyo katika kufanya kazi zake za kila siku huwa ndiyo vinamfanya aweze kutengeneza mambo mazuri zaidi.