Category Archives: Michezo

BAADA YA USHINDI VS KLITSCHKO,ANTONY JOSHUA AMEOMBA PAMBANO LINGINE 

Saa chache tu zimepita tangu kumalizika kwa pambano la ndondi ambapo bondia wa Uingereza Anthony Joshua ameshinda kwa KO vs Klitschko, sasa ametaka pambano dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu Tyson Fury.

Katika interview baada ya pambano vs Wladimir Klitschko wa Ukraine lililopigwa Wembley Stadium, London na kushinda kwa KO round ya 11, Joshua alimuomba Fury ambaye ni Muingereza mwenzie wazichape: “Fury, Tyson Fury, uko wapi baby? Ni hiki unachotaka kuona? Nafurahia kupigana, napenda kupigana.
“Tyson Fury, najua ulikuwa unaongea sana na unataka kurudi na kushindana – nataka kuwapa watu 90,000 nafasi ya kuangalia usiku mwingine wa boxing. Nataka kupigana na kila mtu, nafurahia hii sasa.” – Anthony Joshua.

Naye Tyson Fury baada ya kusikia tambo hizo za Joshua alimjibu kupitia account yake ya twitter akisema amekubali kupambana ambapo aliandika: “Anthony Joshua umekubaliwa. Tutaupa ulimwengu pambano kubwa katika miaka 500. Nitacheza na wewe.” – Tyson Fury.

Advertisements

SIMBA YAIBUKA NA USHINDI WA BAO 1-0 ZIDI YA AZAM

Jumamosi ya April 29 2017 mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Kombe la Azam Sports Federation Cup msimu wa 2016/17 ilichezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa kuzikutanisha timu za Simba dhidi ya Azam FC, huo ukiwa ni mchezo wa tatu kwa timu hizo kukutana kwa mwaka 2017.

Simba leo imefanikiwa kupata ushindi wa kwanza dhidi ya Azam FC kwa mwaka 2017 baada ya kupoteza michezo yao miwili kati ya mitatu waliyocheza dhidi ya Azam FC kwa mwaka 2017, Simba leo imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim dakika ya 48 kwa kutumia vyema pasi kutoka kwa Laudit Mavugo.

Simba sasa inaingia fainali ya Kombe la FA na itakuwa inasubiri mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya kesho kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC mchezo unaochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, kama utakuwa unakumbuka vizuri Simba alipoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC January 13 kwa goli 1-0.

Mchezo wao wa pili kupoteza ukawa uwanja wa Taifa Dar es Salaam January 28 mchezo wa marudiano kwa goli 1-0, kabla ya mchezo wa leo Simba iliifunga Azam FC kwa mara ya mwisho ilikuwa Septemba 17 2016 katika uwanja wa Uhuru mchezo wa round ya kwanza wa Ligi Kuu Vodacom msimu wa 2016/2017.

ZLATAN IBRAHIMOVIC AMEKATAA KULIPWA MSHAHARA NA MAN UNITED

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic amerudi kwenye headlines baada ya maamuzi yake kuandikwa na vyombo vya habari, Zlatan ameripotiwa na mtandao wa dreamteamfc.com kuwa amekataa kulipwa mshahara na Man United.

Zlatan Ibrahimovic atakuwa nje ya uwanja katika kipindi cha miezi 9 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mchezo wa marudiano wa  Europa League dhidi ya Anderltch ya Ubelgiji, Zlatan anayelipwa mshahara wa pound 250000 kwa wiki alijiunga na Man United kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Baada ya kujulikana kuwa Zlatan atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9 Man United walikuwa wapo tayari kuendelea kumlipa mshahara kama kawaida katika kipindi chote cha majeruhi lakini Zlatan amekataa, Zlatan anatarajiwa kurudi uwanja kuanzia mwezi Janury 2018.

KRC GENK INAYOCHEZEWA NA MTANZANIA MBWANA SAMATA IMETOKA SARE YA GOLI 1-1 DHIDI YA AS EUPEN 

Michezo ya Play off ya Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2016/2017 imeendelea tena  April 26 kwa michezo minne kuchezwa KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta walikuwa ugenini kucheza mchezo wao wa 5 wa play off wa Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya wenyeji wao AS Eupen.


KRC Genk waliingia uwanjani kucheza mchezo huo wakiwa wana rekodi ya kuwa timu pekee katika timu 12 zinazocheza game za play off kutofungwa mchezo hata mmoja wakiwa wameshinda michezo yote minne,  leo KRC Genk wakiwa ugenini wamelazimishwa sare ya 1-1 na kuwafanya kupata sare ya kwanza. AS Eupen licha ya kuwa nyumbani walianza kufungwa goli dakika ya 20 Malinovsky akipachika goli la kwanza la Genk lakini AS Eupen walisawazisha goli hilo dakika ya 51, katika michezo ya play off KRC Genk na AS Eupen ndio timu pekee ambazo hazijapoteza mchezo katika timu 12  za Kundi A&B lakini AS Eupen wameshinda game moja pekee kati ya tano.

STAR WA SOKA WA BURNLEY JOE BARTON AMEFUNGIWA MIEZI 18 KUJIUSISHA NA SOKA BAADA YA KUJIUSISHA NA MCHEZO WA BETTING


​Betting ni miongoni mwa michezo inayochukua headlines katika soka kwa siku za hivi, imekuwa ni kawaida kuwaona mashabiki wa soka mbalimbali wakijihusisha na betting, headlines za mchezo wa betting leo zimemgusa staa wa soka wa Burnley Joe Barton.

Staa wa soka wa Burnley aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali vya Ligi Kuu England Joe Barton amefungiwa miezi 18 kujihusisha na soka kutokana na kujihusisha na mchezo wa betting ambapo kwa mujibu wa kazi yake ni kosa kwa sheria za chama cha soka England FA.

                                   Barton

Barton mwenye umri wa miaka 34 amepigwa faini ya pound 30000 na adhabu ya kufungiwa miezi 18 baada ya kuvunja sheria za FA na kujihusisha na betting, Barton alifanya kosa hilo kuanzia March 26 2006-May 13 2016.

Joe Barton ambaye anajiandaa kukata rufaa kutokana na adhabu hiyo kuwa ndefu amekiri kuwa yuko addicted na Betting na atakata rufaa kwa kupeleka FA ripoti ya daktari, Barton pia ameripotiwa kuwahi ku-bet moja kati ya mechi alizocheza kitu ambacho ni kosa na inadaiwa kupelekea upangaji wa matokeo.

SERENGETI BOYS YAWAONESHA UKINARA GABON KWA KUWAFUNGA 2-1 

Timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys  imedhihirisha ubabe wake kwa wenyeji wa fainali za U-17 Afrika mwaka huu, Gabon baada ya kuwafunga tena 2-1 katika mchezo wa kirafiki mjini Rabat.

Mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Assad Juma na Abdul Hussein na hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo vijana wa Tanzania wanawapa wavulana w Gabon, baada ya Aprili 22 kuwafunga pia 2-1, mabao ya Kelvin Nashon Naftali dakika ya 18 na Ibrahim Abdallah Ally dakika ya 75.

Serengeti Boys imeweka kambi ya mwezi mmoja nchini Morocco kujiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17, zinazotarajiwa kuanza Mei 14 hadi 28, mwaka huu nchini Gabon.

Kwa ujumla huo unakuwa mchezo wa tano wa maandalizi kwa Serengeti kujiandaa fainali za Gabon, baada ya awali kuifunga Burundi mara mbili, Machi 30 mabao 3-0 na Aprili 1 mabao 2-0, mechi zote mbili zikipigwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, kabla ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Ghana ‘Black Starlets’ Aprili 3 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti Boys itakuwa kambini mjini Rabat hadi Mei 1, mwaka huu itakapowenda Younde, Cameroon kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya wenyeji Mei 3 na 6, mwaka huu.

Mei 7 timu hiyo itakwenda Gabon ambako imepangwa kundi B pamoja na timu za Mali, Niger na Angola, wakati Kundi A lina timu za wenyeji, Gabon, Guinea, Cameroon na Ghana. 

EMMANUEL OKWI AMEKIRI WANATAKIWA KUFANYA KAZI YA ZIADA KUPATA UBINGWA MSIMU HUU

Uganda. Wakati Ligi Kuu Uganda ikielekea mwishoni, mshambuliaji wa SC Villa, Emmanuel Okwi amekiri wanatakikuwa kufanya kazi ya ziada kupata ubingwa msimu huu.

Pamoja na kukiri kuwa ubingwa utakuwa mgumu kwa kwao kwa sababu  ya kutegemea matokeo ya wapinzani wao,  lakini Okwi amesisitiza kwamba hawawezi kurudi nyuma kwa sababu kimahesabu jambo hilo linawezekana.

SC Villa ipo nafasi ya pili wakitofautiana kwa mabao na vinara KCCA baada ya timu hizo kutoka sare 1-1 mwishoni mwa wiki.

Akizungumza na mtandao wa Kawowo Sports, Okwi alisema walicheza vizuri na kumiliki mpira hata hivyo bahati haikuwa kwao.

“Sasa ni dhahiri ubingwa haupo mikono mwetu, lakini bado kimahesabu tunayo nafasi ya kushinda taji msimu huu.”

“Sitaki kuzungumza sana, lakini ni dhahiri hatukuwa na bahati na mwishowe tulipata sare. Tunatarajia kushinda michezo mingine inayofuata.”

Okwi alisawazishia Villa kwa bao la shuti la umbali wa mita 12 na kufuata bao la awali la KCCA lililofungwa na Geofrey Sserunkuma.

Villa sasa italazimika kuomba dua baya kwa KCCA ilipoteza mechi zake zilizosalia na wenyewe kushinda mechi zilizosalia ili kujihakikishia kutwaa ubingwa msimu huu.

KUPOLWA POINT TATU NI SABABU ZITAKAZOCHANGIA KUVULUGA MIPANGO YA SIMBA NA HARAKATI ZAKE ZA KUSAKA UBINGWA LIGI KUU 


Kitendo cha kufungwa na Kagera, sare dhidi ya Toto Africans, kupolwa pointi tatu zimetajwa kuwa sababu zitakazochangia kuvurugika kwa mipango ya Simba na harakati zake za kusaka ubingwa msimu huu.

Wachambuzi wa masuala ya soka nchini wanabainisha kuwa timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi inaweza kusubiri bahati, ama kutuliza kisaokolojia kikosi chake ili iwe bingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Uongozi wa klabu na benchi la ufundi la klabu hiyo wameambiwa wasake tiba ya haraka ya kisaikolojia kwa wachezaji wao na wasiwavuruge kwa mambo yanayoendelea ndani ya klabu ili wapate matokeo katika michezo mitatu iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema kila kitu kinakwenda sawa na masuala ya nje ya uwanja, yanayoendelea hivi sasa yameachwa kwa uongozi na akili ya wachezaji ni mechi zao zilizosalia kwenye Ligi Kuu na Kombe la FA.

Mchambuzi wa masuala ya michezo, Jeff Lea, alisema: “Tofauti ya pointi na Yanga ni tatu, lakini Yanga ina michezo miwili mkononi, kitu ambacho kinaipa Simba wakati mgumu kutwaa ubingwa, labda itokee bahati ya mtende.

“Kwangu mimi ninaona labda ielekeze nguvu katika FA na ifuzu kucheza fainali, hapo itakuwa imefufua matumaini ya kushiriki mashindano ya kimataifa, lakini kwenye ligi itachukua taji hilo kwa bahati.”

Mchambuzi mwingine, Ally Mayay alisema bado anaamini nafasi ya ubingwa ipo wazi kwa Simba kama ikishinda mchezo dhidi ya African Lyon, ambao anauona ndiyo mgumu zaidi kwa timu hiyo.

“Kitu ambacho unacho mkononi ni bora kuliko ambacho huna, Yanga haijapata bado pointi ingawa ina michezo miwili mkononi, tofauti na Simba ambayo ina pointi, lolote linaweza kutokea kwa Yanga.

“Kinachotakiwa ni Simba kutulia na kushinda mchezo wa Lyon, ambayo ina nyota wengi walioichezea Simba, lakini pia inacheza kwa kuangalia matokeo ya Yanga,” alisema Mayay.

Kocha na mchambuzi wa soka, Joseph Kanakamfumu alisisitiza kuwa ubingwa kwa Simba upo wazi, lakini wakitulia na wachezaji kupewa tiba ya saikolojia.

Simba imebakisha mechi tatu, ambazo ikishinda itafikisha pointi 68 ikilinganishwa na Yanga iliyobakisha michezo mitano kabla ya msimu kumalizika, ambayo kama itashinda yote itafikisha pointi 71 ingawa timu zote pia zimetinga nusu fainali ya Kombe la FA.     

KOCHA WA MBAO FC AMESEMA ANATAKA KUWEKA ESHIMA KOMBE LA FA

Wakati makocha wa Simba, Yanga na Azam kila mmoja akitaka rekodi kwenye Kombe la Shirikisho, mwenzao wa Mbao, Etienne Ndayiragije anapigia hesabu ya kuweka heshima.

Timu hizo zitavaana katika nusu fainali kwa Simba kucheza na Azam Jumamosi jijini Dar es Salaam katika nusu fainali ya kwanza, wakati Mbao FC ikiwa nyumbani, CCM Kirumba dhidi ya Yanga, Jumapili katika nusu fainali ya pili.

Kwa nyakati tofauti jana, makocha wa timu hizo, walielezea mikakati yao kuelekea kwenye michezo hiyo na bingwa licha ya kuondoka na kitita cha Sh 50 milioni ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Shirikisho Afrika mwakani.

Kocha msaidizi wa Azam, Idd Cheche alisema mipango ya klabu yao ni kutwaa ubingwa huo na kusisitiza kwamba, kikosi chao kimeanza kambi tangu jana tayari kuikabili Simba katika nusu fainali.

“Timu itaingia kambini jioni ya leo (jana) kwenye uwanja wetu wa Chamazi kwa ajili ya maandalizi ya FA, tunajua ugumu wa mchezo huo lakini tutapambana,” alisema Cheche.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema timu yao imeanza mazoezi siku nne zilizopita kwa ajili ya mchezo huo ambao ameutaja kuwa muhimu kwa timu yao.

“Mechi ya Jumamosi ni muhimu kwa Simba, tunahitaji ushindi huo hatimaye kucheza fainali na kuwa mabingwa, tunatambua umuhimu wa mchezo na benchi letu la ufundi linaendelea na kazi,” alisema Mgosi.  

MTANZANIA ALPHONSE SIMBU APONGEZWA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGELEZA DKT ASHA ROSE MIGIRO LEA KUSHIKA NAFASI YA TANO KTK MBIO ZA LONDON MARATHON

Tarehe 24 Aprili, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Dkt. Asha Rose Migiro aliandaa hafla fupi katika makazi ya Balozi kumpongeza kijana mtanzania Alphonse Simbu Kwa kushika nafasi ya ya tano(5) katika mbio za “London Marathon” zilizofanyika tarehe 23 Aprili 2017 jijijini London.

Katika salamu zake,Balozi Migiro alimpongeza Bw.Simbu kwa heshima aliyoipa Tanzania jijini London na Duniani kupitia mbio za London.

Aisha alimsihi atumie matokeo hayo kama hamasa ya kufanya bidii zaidi kwa ajili ya mashindano ya mbio ndefu anayotarajiwa kushiriki baadae mwakani.

Bw.Simbu alimshukuru Balozi Migiro Kwa ushirikiano mkubwa wa kibalozi alioupata akiwa jijini London.Alimkabidhi Balozi Fulana ya kumbukumbu ya ushiriki wake kwenye mbio hizo.

Pichani Balozi Asha Rose Migiro akipokea Fulana hiyo. 

#Tanzania