Category Archives: Mataifa

TRUMP ASISITIZA HACHUNGUZWI NA FBI

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hachunguzwi  na mtu yeyote wala shirika la ujasusi la FBI halimchunguzi. Hiyo ni baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la FBI.
Akizungumza na chombo cha habari cha NBC jana, Trump alisema  kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.

Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya maofisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.

Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliyopingwa na mrithi wa Comey.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo, Trump aliiambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza Comey iwapo alikuwa akimchunguza.

“Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia, huchunguzwi.” alisema Trump

Advertisements

RAIS MPYA MOON JAE-IN WA KOREA KUSINI APANGUA VIONGOZI

Lee Nak-yon, Mkuu wa Mkoa wa Jeolla Kusini, ametajwa kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Rais Moon. Uteuzi wake utawasilishwa katika Bunge la nchi hiyo na ataanza kutekeleza majukumu yake baada ya kupitishwa na wabunge.
Korea Kusini. Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini aliyechaguliwa juzi, amefanya mabadiliko makubwa katika safu ya uongozi akiwateua waziri mkuu mpya, mkuu wa shirika la ujasusi, mnadhimu mkuu wa Ikulu na mkuu wa huduma ya usalama wa Rais. 

Lee Nak-yon, Mkuu wa Mkoa wa Jeolla Kusini, ametajwa kuwa Waziri Mkuu katika Serikali ya Rais Moon. Uteuzi wake utawasilishwa katika Bunge la nchi hiyo na ataanza kutekeleza majukumu yake baada ya kupitishwa na wabunge.@ 

Rais Moon pia amemteua Im Jong-seok kuwa Mnadhimu Mkuu wa Ikulu, huku Suh Hoon akiteuliwa kuchukua wadhifa wa mkuu wa shirika la ujasusi la Korea Kusini.

COM WATIMUANA TENA ARUSHA 

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewafukuza viongozi wake katika kata nne kwa tuhuma mbalimbali ikiwepo matumizi mabaya ya fedha na mali za chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa, Hamfrey Polepole ametangaza leo uamuzi huo na kuelezea CCM haitawavulia wanachama wake wabadhirifu

Viongozi waliofukuzwa na wa kata za Themi, Sombetini, Unga LTD na  Sekei.

BREAKING:MTANDAO WA WHATSAPP UMEPOTEA HEWANI DUNIA NZIMA

Inawezekana wewe ukawa ni mmoja kati ya watu ambao wameshangazwa na kuona simu zao usiku huu ukituma ujumbe wa Whatsapp hauendi na kuanza kujiuliza kama shida ni salio, simu au tatizo la kiufundi.

Taarifa ikufikie kuwa tatizo hilo limetokea na kwa mujibu wa msemaji wa mtandao huyo” baadhi ya watu wamepata tatizo la kushindwa kupata huduma ya whatsapp kwa leo, tunaomba radhi kwa usumbufu na tunashughulikia kuhakikisha huduma hiyo inarejea mapema”

Mtandao huo wa Whatsapp hauko hewani dunia nzima sababu za kutokuwa hewani bado hazijawekwa wazi kama tatizo ni nini 

ZLATAN IBRAHIMOVIC AMEKATAA KULIPWA MSHAHARA NA MAN UNITED

Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic amerudi kwenye headlines baada ya maamuzi yake kuandikwa na vyombo vya habari, Zlatan ameripotiwa na mtandao wa dreamteamfc.com kuwa amekataa kulipwa mshahara na Man United.

Zlatan Ibrahimovic atakuwa nje ya uwanja katika kipindi cha miezi 9 baada ya kuumia goti lake la kulia wakati wa mchezo wa marudiano wa  Europa League dhidi ya Anderltch ya Ubelgiji, Zlatan anayelipwa mshahara wa pound 250000 kwa wiki alijiunga na Man United kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Baada ya kujulikana kuwa Zlatan atakuwa nje ya uwanja kwa miezi 9 Man United walikuwa wapo tayari kuendelea kumlipa mshahara kama kawaida katika kipindi chote cha majeruhi lakini Zlatan amekataa, Zlatan anatarajiwa kurudi uwanja kuanzia mwezi Janury 2018.

PAPA FRANCIS KUZUNGUMZIA MAUSIANO YA KIDINI MISRI


​Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis anaelekea nchini Misri hii leo kwa ziara fupi inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidini na ulimwengu wa Kiislamu.
Ziara hiyo inajiri wakati ambapo kuna ongezeko la mauaji ya Wakristo waliopo katika mashariki ya kati hususan wale wa jamii ya kanisa la Coptic.
Mapema mwezi huu kundi la Islamic state lilikiri kutekeleza shambulio la mabomu ya makanisa mawili ya Coptic.
Papa Francis atakutana na rais wa Misri   ili kutoa hotuba kuhusu amani katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar, taasisi ya masomo ya Kiislamu miongoni mwa madhehebu ya Sunni.

MAGARI YANAYO PAA KUJA MWAKA 2020 


Dira ya Dunia ya BBC Swahili usiku wa April 26 2017 ambapo ipo taarifa ya Uber kuja kuzindua magari yanayopaa angani ifikapo mwaka 2020.
Magari hayo ya umeme yatapaa angani na kutuwa yakiwa wima bila kuchafua mazingira na hayatakuwa na sauti kubwa huku gharama yake ikiwa ni sawa na teksi za kawaida, pamoja na hiyo taarifa zipo na habari nyingine kama ulizikosa ndo time yako ya kuzitazama.

WATU 24 WAMEFARIKI KATIKA AJALI KENYA 

Watu 24 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa manane katika barabara kuu ya kutoka Nairobi kwenda Mombasa.

Ajali hiyo iliyohusisha basi la kubeba abiria na lori la kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kiambu, karibu na Mtito Andei.

Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard Kimaiyo ameambia BBC kuwa watu 23 walifariki papo hapo na mwingine mmoja alifariki alipokuwa akipata matibabu.

Watu 20 walipata majeraha na kupelekwa katika hospitali za miji ya Kibwezi na Makindu.

 Kimaiyo amesema walionusurika waliwaambia maofisa wa polisi kuwa dereva wa basi alikuwa akijaribu kupita gari jingine na kusababisha basi hilo kugongana na lori hilo.

Kwa mujwibu wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi Kenya, watu 3,000 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.