Category Archives: Filamu

MAMBO MATANO ALIYO YASEMA RAY KIGOSI YA DIAMOND NA MAREHEMU KANUMBA KUAMBIWA NI MA FREEMASON 

Muigizaji staa wa Bongo movie Ray Kigosi ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopata mafanikio makubwa kwenye industry ya filamu nchini na kufanikiwa kujijengea jina na heshima kwa jamii.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray ametoa ujumbe ambao unalenga kutoa uelewa kwa mashabiki hasa wa filamu na muziki nchini ambao wamekuwa wakiwahusisha baadhi ya mastaa wanaofanya vizuri na imani tofauti.
Katika kuufikisha ujumbe huo Ray amewatolea mfano staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz na muigizaji nyota Stiven Kanumba aliyefariki miaka mitano iliyopita ambaye alifanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie.
Ray Kigosi ameandika…
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!
2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!
3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.

Anadai alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO

Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.
5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.
Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.

Advertisements

MUIGIZAJI NA MCHEKESHAJI MAARUFU STEVE NYERERE AMUOMBEA MSAMAHA NEY WA MITEGO 

Akizungumza leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Steve Nyerere amesema kwamba yawezekana  Nay wa Mitego alikuwa na hasira hivyo akashindwa kutumia lugha sahihi ya kuwaelekeza wasanii wenzake walivyokuwa wanakosea ndio maana alitoa lugha yenye maneno makali ijapokuwa alikuwa sahihi kukosoa maandamano yale.
“Kwanza naomba nimuombee msamaha ndugu yangu Nay wa Mitego, hakuwa na nia mbaya lakini hakutumia maadili kufikisha ujumbe wake, Unajua sisi watanzania hatupendi kuambiwa ukweli na hata tukisemana tuna lugha zetu laini za kusemeshana. Nay wa Mitego mpaka kutoa maneno makali vile ujue anaipenda tasnia yetu ya filamu alikuwa kaaumia, si unajua hata yeye alishawahi kuwa huku anatuonea huruma na anatupenda mimi niseme mumsamehe tuu” – alisema Steve.

Aidha Steve Nyerere ameongeza kuwa kwa hali ilivyo katika tasnia ya filamu Tanzania hakuna haja ya maandamano pamoja na kurushiana maneno kwenye mitandao bali kinachotakiwa ni kukalishana chini waigizaji wote na kuangalia mahali walipojikwaa na kufanya marekebisho.

“Mtandaoni hatutaweza kumaliza hili tatizo kinachotakiwa hapa ni tukae chini na tuongee tunataka nini. Msibague kuandamana kwa ajili ya faida yenu wenyewe ila tujenge hoja ambayo tukubaliane wote tuiombe serikali itusaidie wote kwa ujumla na siyo watu wachache wanaojifanya manabii hawataki kukosolewa” Steve Nyerere alisistiza.