Category Archives: Buludani

WASANII WAMJIA JUU MWAKYEMBE KUHUSU KUJIHUSISHA NA SIASA 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amejipalia makaa.
Onyo lake dhidi ya kuchanganya siasa na muziki, limewasha moto na sasa anashambuliwa nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano na wasanii ambao wanasema ni jambo lisilowezekana kutofautisha mawili hayo.

Dk Mwakyembe, ambaye aliteuliwa hivi karibuni kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuchukua nafasi ya Nape Nnauye aliwataka wasanii kuachana na nyimbo zinazoishambulia Serikali au viongozi na kuwataka wachague ama kuwa wasanii au wanasiasa.

Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Mikumi (Chadema), Joseph Haule, ambaye pia ni mwanamuziki wa rap akijulikana kwa jina la Profesa J, kuwa wasanii wanaoiimba nyimbo za siasa kuihoji Serikali wamekuwa wakinyanyaswa. Dk Mwakyembe alisema wakati akijibu swali hilo kuwa wasanii waelekeze tungo zao kwenye burudani si siasa. Juzi, mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, ambaye kisanii anajulikana kama Sugu, alisema imefika wakati kwa Dk Mwakyembe kujiwekea utaratibu wa kusoma na kufanya tafiti za kina kabla ya kutoa kauli ambazo hazitekelezeki.

Alisema kumpangia mwanamuziki atunge au aimbe nini, ni jambo lisilowezekana kwa kuwa tungo nyingi ni zao la maisha halisi ya jamii ambayo mwanamuziki husika anatokea.

“Sitashangaa kusikia kauli hiyo imetenguliwa. Hili ni jambo la ajabu ndiyo sababu limetushangaza wengi. Muziki ndiyo silaha ya kwanza ya ukombozi na haiwezekani kumpangia mwanamuziki atunge au aimbe kuhusu nini,” alisema Sugu ambaye aliibuka kwa kuimba nyimbo za rap zenye ujumbe wa siasa.

“Inawezekana vipi tu juzi aseme kuwa Rais ameruhusu wimbo wa Nay (wa Mitego) upigwe redioni na kusisitiza kuwa yupo huru atunge nyimbo nyingine, halafu leo anakuja kusema kuwa mwanamuziki asiimbe nyimbo za siasa? Ndiyo sababu nina imani kauli hii nayo itakuja kufutwa,” alisema Mbilinyi.

Hoja hiyo haikuwa tofauti sana na iliyotolewa na mwanamuziki kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili aliyesema kuwa sanaa ni mali ya msanii na mara zote anaimba kutokana na uzoefu wake wa kile kinachoendelea kwenye jamii.

Alisema licha ya kuwapo kwa mgongano wa muda mrefu kati ya Serikali na sanaa, ni vigumu kutenganisha siasa na sanaa kwa kuwa vimekuwa vikishirikishana.

“Sanaa imekuwa ikitumika kufanya harakati za ukombozi na siasa. Hakuna namna ambavyo unaweza kuzuia sanaa isiingie kwenye siasa kwa kuwa ina mchango mkubwa upande huo. Naweza kusema sanaa na siasa ni mapacha wa miaka mingi,” alisema Nikki.

Kauli kama hiyo ilitolewa na Nay wa Mitego, ambaye aliwahi kukamatwa kwa wimbo wake wa “Wapo”, aliyesema muziki na siasa ni maisha ya mwanadamu.

“Nadhani waziri mwenyewe atakuwa na majibu ya kina kuhusu alichokisema. Huenda ana nia njema ya kutuepusha vijana wake kwenye hatari kwa mujibu wa hali anavyoiona. Ila binafsi naamini naimba muziki unaogusa maisha halisi ya jamii niliyopo,” alisema.

Muigizaji wa filamu Shamsa Ford alisema kauli hiyo ya waziri inalenga kuwanyima haki wasanii kushiriki kwenye siasa ilhali nao ni sehemu ya jamii.

“Msanii naye ana haki ya kupiga kelele kwa masilahi ya Taifa lake. Anapoona jambo haliendi sawa ni jukumu lake kupaza sauti, kwa nini tuzuiwe. Kama hufanyi uchochezi sioni sababu ya kuwekewa mipaka,” alisema Shamsa.

Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (Taff), Simon Mwakifwamba alisema ipo haja ya sanaa kuangaliwa kwa mapana yake kwa kuwa ina nafasi ya kujenga au kubomoa jamii.     

Advertisements

BAADA YA CHIBU PERFUME ..ALIKIBA ATANGAZA BIDHAA ATAZOLETA

Habari njema za Mastaa wa bongo kutengeneza njia za kujiongezea kipato zaidi kwa kutengeneza bidhaa zenye majina yao zinaendelea kuongezeka ambapo leo ni zamu ya Alikiba.
Zikiwa zimepita wiki mbili toka Mwimbaji mwingine staa wa Bongofleva Diamond Platnumz kuzindua Perfume yake, leo May 11, 2017 kupitia 255 ya XXL Mwimbaji staa wa ‘aje’ Alikiba ameweka wazi kuwa moja ya mipango yake ni kutoa mavazi aina ya jeans, miwani, viatu na vinywaji vya energy vyenye jina lake.

Alikiba amesema kuwa hiyo ni mipango mizito na hatarajii kuifanya kiholela kwani hata mwanzo alifanya kama promotion lakini sasa hivi hayupo tayari kuikosea serikali na amejipanga kufungua na duka ili watu wake waweze kupata kwa urahisi.

“AK ni Brand ya Alikiba nashukuru imekuwa kubwa watu wanavaa lakini pia ipo na ya King Kiba nayo ni brand yangu na zipo official kabisa na kazi zitakapoanza watapata product zote’ – Alikiba

“Kuna Malengo makubwa sana tumeyaweka lakini siwezi kusema sasa hivi ila kuna Jeans Viatu na Glasses tayari zishatoka soon wataziona maana hizi zitakuwa za kwanza sababu tayari zishatoka na kuna energy drink” – Alikiba

SHILOLE ASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI 

Msanii wa muziki wa kizazi wa Bongo Fleva na filamu, nchini Zuwena Mohamed maarufu kama  Shilole ameshindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi katika kesi ya matumizi mabaya ya mtandao kwa kuwa anaumwa.
Leo (Jumatano) Shilole alipaswa kutoa ushahidi katika kesi hiyo inayomkabili mwanafunzi wa Chuo cha Bandari, Thomas Lucas (20) inayosikilizwa mbele ya Hakimu Boniface Lyamwike.

Katika kesi hiyo, Lucas anakabiliwa na shtaka la mtandao kwa kumkashfu Shilole kupitia kwenye mtandao wa Instagram.

Inadaiwa  kuwa mshtakiwa huyo alifanya hivyo wakati akijiua ni kosa na kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya mtandao namba 14 ya 2016.

Hata hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,2017 ambapo itaendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

BAADA YA USHINDI VS KLITSCHKO,ANTONY JOSHUA AMEOMBA PAMBANO LINGINE 

Saa chache tu zimepita tangu kumalizika kwa pambano la ndondi ambapo bondia wa Uingereza Anthony Joshua ameshinda kwa KO vs Klitschko, sasa ametaka pambano dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu Tyson Fury.

Katika interview baada ya pambano vs Wladimir Klitschko wa Ukraine lililopigwa Wembley Stadium, London na kushinda kwa KO round ya 11, Joshua alimuomba Fury ambaye ni Muingereza mwenzie wazichape: “Fury, Tyson Fury, uko wapi baby? Ni hiki unachotaka kuona? Nafurahia kupigana, napenda kupigana.
“Tyson Fury, najua ulikuwa unaongea sana na unataka kurudi na kushindana – nataka kuwapa watu 90,000 nafasi ya kuangalia usiku mwingine wa boxing. Nataka kupigana na kila mtu, nafurahia hii sasa.” – Anthony Joshua.

Naye Tyson Fury baada ya kusikia tambo hizo za Joshua alimjibu kupitia account yake ya twitter akisema amekubali kupambana ambapo aliandika: “Anthony Joshua umekubaliwa. Tutaupa ulimwengu pambano kubwa katika miaka 500. Nitacheza na wewe.” – Tyson Fury.

U-HEARD NDOA YA NUH MZIWANDA YATAKIWA KUFUNGWA TENA 

Ni siku moja tu imepita tangu staa wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda kupitia account ya Instagram kupost picha ya mtoto wake aliyebarikiwa katika ndoa yake, inadaiwa ndoa hiyo kuingia katika mvutano.
Inasemekana kuwa ndugu wa Nuh Mziwanda hawakuridhia ndoa ya ndugu yao iliyofungwa miezi kadhaa iliyopita kwa kuwa Nuh alibadili dini kufuata dini ya mke wake ambapo kupitia U-heard  ya XXL ya Clouds FM April 28 2017 mtangazaji Soudy Brown ameinasa sauti ya mke wa Nuh Mziwanda akimzungumza mama mkwe wake:
“Nilimwambia mama unachelewa, mwambie aniache. Na anajua kuwa mimi sijaolewa na mwanawe, ila anajua nimezaa tu na mwanawe. Kwenye sherehe ya harusi hakuwepo, alikuwa kwenye msiba. Yule mama ni mzee wa Kanisa, alikuwa anataka niende kanisani nibadili dini ndio niolewe.” – Mama ANYA

MSANII WA FILAMU NICOLE ALALAMIKA KUIBIWA BWANA NA VANESA MDEE

Msanii wa filamu nchini Nicole aliyezaa na mbunge ambaye hakutaka kuweka jina lake wazi amefunguka tetesi za mzazi mwenzake huyo kutoka kimapenzi na msanii Vanessa Mdee na kusema yeye anafahamu kuwa Vanessa na mzazi mwenzake huyo ni kama mtu na mdogo

 

                  Msanii wa filamu Nicole.

Akiongea kwenye kipindi cha eNewz Nicole amedai yeye hafahamiani kabisaa na Vanessa Mdee anasema anamjua kama msanii ila anatambua kuwa mzazi mwenzake huyo ambaye ni mbunge yupo karibu na msanii huyo wa bongo fleva. 

“Mimi nasikia tu stori lakini mimi na huyo mwanaume tumeshaachana tayari na kuachana kwetu siyo sababu ya Vanessa. Huyo Vanessa mimi simfahamu zaidi ya kumuona tu kwenye tv kwa hiyo siwezi kumnunia kwa sababu yeye ni mwanamke kama wengine na kama amependwa pia sio mbaya ila mimi nilimuuliza pia mzazi mwenzangu baada ya kusikia na akasema kuwa hana mahusiano naye ila anamchukulia kama mdogo wake. Kwa hiyo mimi na mzazi mwenzangu bado tunawasiliana kwa sababu tuna mtoto pamoja ” alisema Nicole 

Nicole ni moja kati ya waigizaji wa bongo movie ambao wanafanya vizuri na sasa ni mama wa mtoto mmoja ambaye amezaa na mbunge. 

DIAMOND AMUANDIKIA UJUMBE RAY C KUPITIA UKURASA WAKE WA INSTAGRAM 

​Ikiwa ni siku chache baada ya Mwimbaji Ray C kuachia wimbo wake wa Unanimaliza, Leo Msanii wa BongoFleva, Diamond Platnumz kupitia account yake ya Instagram ameandika ujumbe huu…..
Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali….
Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya…. Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….
niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku