NBS IMEKANUSHA TAARIFA ZILIZOSAMBAA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUWA UPIMAJI WA UKIMWI NYUMBA KWA NYUMBA

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekanusha taarifa zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa upimaji wa Ukimwi nyumba kwa nyumba utaanza mwishoni mwa mwezi huu.
Taarifa hiyo iliyosambaa hivi karibuni ilimnukuu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Grace Magembe ikisema, “Upimaji wa VVU nyumba kwa nyumba sasa rasmi, mchakato unaendelea na zoezi litaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu.”

Hata hivyo kupitia taarifa yake kwa umma NBS imefafanua kuwa Ukimwi haupimwi nyumba kwa nyumba  bali unafanyikia utafiti wa viashiria na matokeo ya Ukimwi na kwamba utafiti huo utafanyika kwa kaya chache zilizochaguliwakitaalamu nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine.

Utafiti huo utahusisha kaya 16,000 ambazo ni sampuli  iliyochaguliwa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Zanzibar.

Taarifa hiyo imesema kwa Dar es Salaam utafiti huo wa viashiria na matokeo ya Ukimwi utahusisha kaya zisizozidi 1,000 na unatarajia kuanza Mei 21 mwaka huu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s