WENYE SIFA KUFURAHIA AJIRA TANZANIA 

Baada ya Rais John Magufuli kuagiza watumishi waliobainika kutumia vyeti vya kughushi waondoke katika maeneo yao ya kazi mara moja kabla hawajaadhibiwa kwa mujibu wa sheria, imeelezwa kuwa hiyo inaweza kuwa neema kwa vijana wasomi wasiokuwa na ajira.

Rais Magufuli alisema hayo alipokuwa akipokea ripoti ya uhakiki wa vyeti feki mjini Dodoma baada ya kukamilika kwa uhakiki uliofanyika kwa miezi sita na watumishi 9,932 wakigundulika kutumia vyeti feki huku wengine 1,538 wakitumia cheti kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja.

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini (CEOrt), Ali Mufuruki amesema kwa kufanya hivyo Serikali inaweka viwango bora vya elimu.

Pia, amesema inatoa nafasi kwa waliokuwa na elimu bora angalau kuingia kwenye soko la ajira, kwa sababu kuna nafasi zipo wazi zinazotakiwa kujazwa na wale tu wenye sifa.
 “Hii ni alarm hata kwa sisi sekta binafsi, kuliangalia hili kwa kina na kuongeza umakini wakati wa kuajiri, ”amesema Mufuruki.

Mufuruki anaungwa mkono na Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Humphrey Moshi aliyesema waliofukuzwa watafungua mianya kwa wenye vyeti sahihi ambao hawajaajiriwa.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s