JPM AWASAMEHE WANANCHI WA HAI

Rais John Magufuli  amewaambia wakazi wa mji wa Bomang’ombe katika Jimbo la Hai kuwa amewasamehe.

Alitoa kauli hiyo akiwa katika jimbo hilo la Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe baada ya kuwaona baadhi ya wananchi wakiwa wameshika jani la “Sale” ambalo hutumiwa na wenyeji kuomba msamaha.

Jani hilo linaloheshimiwa sana na wachaga wa mkoa huo, ndilo ambalo mtu akimpelekea mtu aliyemkosea na kumuomba yaishe, anayeombwa kupitia jani hilo hana jinsi lazima akubali.

“Nawashukuru sana wote mliokuja na haya majani ya mti. Nafahamu maana yake na mimi nimewasamehe wote. Najua na ninyi mmenisamehe wote,”amesema Rais Magufuli huku akishangiliwa.

Ingawa Rais Magufuli hakuweka bayana walichomkosea, lakini katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015, Rais Magufuli alipata kura 29,341 wakati mpinzani wake wa karibu, Edward Lowassa akipata kura 49,125.

“Tushikamane kwa pamoja tujenge nchi yetu. Hakuna Mtanzania anayekula vyama, Mtanzania anataka maendeleo, anataka hospitali, barabara, anataka madawa, maji yapatikane umeme,”alisema Rais.

“Hii ndio maana niko hapa kwa ajili yenu, naomba mniamini na Serikali yangu tuko kwa ajili ya kuijenga Hai na Tanzania kwa ujumla. Aika mae, Aikambe (Asanteni sana),”alisisitiza Rais Magufuli.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Jimbo hilo kwa kura alizosema ni nyingi na ambazo zilimuwezesha kuwa Rais na akawaahidi kuwa atawaletea maendeleo bila kujali vyama.

“Ninawashukuru sana nataka niwaahidi mimi nitawafanyia kazi Watanzania wote bila kujali vyama vyao, bila kujali makabila yao, bila kujali dini zao bila kujali hata sura zao,” alisema.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s