SIKU YA MALARIA DUNIANI NA CHANJO ZAKE


​Leo ni siku ya Malaria duniani. Tanzania na nchi nyingine za Afrika zimeendelea kupamba na ugonjwa huu wakati chanjo yake ikiendelea kufanyiwa majaribio.

Shirika la Afya Duniani WHO limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu ya maisha, huku malari ikiendelea kupoteza maisha ya watu.

Mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi ya watoto 700,000 wenye umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na nusu.

Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia mia moja, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Hii inafuata miongo kadhaa ya tafiti ya kutafuta ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo duniani.

Chanjo hiyo mpya, itakwenda sambamba na hatua nyengine za kujikinga kama vile neti, dawa za kufukuza mbu, na dawa za kukinga malaria.

Wakati wa majaribio, maelfu ya watoto watapewa chanjo hiyo mara nne katika kipindi cha miaka miwili.
 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s