KUPOLWA POINT TATU NI SABABU ZITAKAZOCHANGIA KUVULUGA MIPANGO YA SIMBA NA HARAKATI ZAKE ZA KUSAKA UBINGWA LIGI KUU 


Kitendo cha kufungwa na Kagera, sare dhidi ya Toto Africans, kupolwa pointi tatu zimetajwa kuwa sababu zitakazochangia kuvurugika kwa mipango ya Simba na harakati zake za kusaka ubingwa msimu huu.

Wachambuzi wa masuala ya soka nchini wanabainisha kuwa timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi inaweza kusubiri bahati, ama kutuliza kisaokolojia kikosi chake ili iwe bingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Uongozi wa klabu na benchi la ufundi la klabu hiyo wameambiwa wasake tiba ya haraka ya kisaikolojia kwa wachezaji wao na wasiwavuruge kwa mambo yanayoendelea ndani ya klabu ili wapate matokeo katika michezo mitatu iliyosalia kabla ya kumalizika kwa msimu.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema kila kitu kinakwenda sawa na masuala ya nje ya uwanja, yanayoendelea hivi sasa yameachwa kwa uongozi na akili ya wachezaji ni mechi zao zilizosalia kwenye Ligi Kuu na Kombe la FA.

Mchambuzi wa masuala ya michezo, Jeff Lea, alisema: “Tofauti ya pointi na Yanga ni tatu, lakini Yanga ina michezo miwili mkononi, kitu ambacho kinaipa Simba wakati mgumu kutwaa ubingwa, labda itokee bahati ya mtende.

“Kwangu mimi ninaona labda ielekeze nguvu katika FA na ifuzu kucheza fainali, hapo itakuwa imefufua matumaini ya kushiriki mashindano ya kimataifa, lakini kwenye ligi itachukua taji hilo kwa bahati.”

Mchambuzi mwingine, Ally Mayay alisema bado anaamini nafasi ya ubingwa ipo wazi kwa Simba kama ikishinda mchezo dhidi ya African Lyon, ambao anauona ndiyo mgumu zaidi kwa timu hiyo.

“Kitu ambacho unacho mkononi ni bora kuliko ambacho huna, Yanga haijapata bado pointi ingawa ina michezo miwili mkononi, tofauti na Simba ambayo ina pointi, lolote linaweza kutokea kwa Yanga.

“Kinachotakiwa ni Simba kutulia na kushinda mchezo wa Lyon, ambayo ina nyota wengi walioichezea Simba, lakini pia inacheza kwa kuangalia matokeo ya Yanga,” alisema Mayay.

Kocha na mchambuzi wa soka, Joseph Kanakamfumu alisisitiza kuwa ubingwa kwa Simba upo wazi, lakini wakitulia na wachezaji kupewa tiba ya saikolojia.

Simba imebakisha mechi tatu, ambazo ikishinda itafikisha pointi 68 ikilinganishwa na Yanga iliyobakisha michezo mitano kabla ya msimu kumalizika, ambayo kama itashinda yote itafikisha pointi 71 ingawa timu zote pia zimetinga nusu fainali ya Kombe la FA.     

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s