KOCHA WA MBAO FC AMESEMA ANATAKA KUWEKA ESHIMA KOMBE LA FA

Wakati makocha wa Simba, Yanga na Azam kila mmoja akitaka rekodi kwenye Kombe la Shirikisho, mwenzao wa Mbao, Etienne Ndayiragije anapigia hesabu ya kuweka heshima.

Timu hizo zitavaana katika nusu fainali kwa Simba kucheza na Azam Jumamosi jijini Dar es Salaam katika nusu fainali ya kwanza, wakati Mbao FC ikiwa nyumbani, CCM Kirumba dhidi ya Yanga, Jumapili katika nusu fainali ya pili.

Kwa nyakati tofauti jana, makocha wa timu hizo, walielezea mikakati yao kuelekea kwenye michezo hiyo na bingwa licha ya kuondoka na kitita cha Sh 50 milioni ataiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Shirikisho Afrika mwakani.

Kocha msaidizi wa Azam, Idd Cheche alisema mipango ya klabu yao ni kutwaa ubingwa huo na kusisitiza kwamba, kikosi chao kimeanza kambi tangu jana tayari kuikabili Simba katika nusu fainali.

“Timu itaingia kambini jioni ya leo (jana) kwenye uwanja wetu wa Chamazi kwa ajili ya maandalizi ya FA, tunajua ugumu wa mchezo huo lakini tutapambana,” alisema Cheche.

Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’ alisema timu yao imeanza mazoezi siku nne zilizopita kwa ajili ya mchezo huo ambao ameutaja kuwa muhimu kwa timu yao.

“Mechi ya Jumamosi ni muhimu kwa Simba, tunahitaji ushindi huo hatimaye kucheza fainali na kuwa mabingwa, tunatambua umuhimu wa mchezo na benchi letu la ufundi linaendelea na kazi,” alisema Mgosi.  

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s