MASHINDANO YA UBINGWA WA TAIFA 2017 YATAANZA KESHO 25/04/2017

Mashindano ya ubingwa wa Taifa 2017 yataanza kesho  Tarehe 25/04/2017 katika viwanja vya wazi  vya Tanganyika packers Kawe jijini Dar es salaam, kabla ya kuanza rasmi, litaanza zoezi la kupima uzito na afya kwa mabondia wote waliojiandaa kushiriki mashindano hayo.

Tukio la kupima uzito na afya litafanyika katika enoa la mashindano Kawe Tanganyika packers kuanzia saa 1.00- 4.00 Asubuhi, Baada ya hapo saa 5.00- 6.00 kutakuwa na tukio la kutayarisha ratiba nzima ya mashindano kwa mabondia wote watakaokuwa wamefuzu zoezi la kupima uzito na afya . Kuanzia saa 8.00 Mchana tunategemea kuanza rasmi mashindano.

Aidha mkutano mkuu uliokuwa ufanyike leo tarehe 24/04/2017 umeshindwa kufanyika  kutokana na akidi kutofikia idadi inayotakiwa kwa mujibu wa katiba ya BFT. Kutokana na hilo Rais wa BFT Mutta Rwakatare aliahirisha Mkutano huo na kutangaza utafanyika  Tarehe nyingine baada ya kujipanga upya.

Shirikisho linawaomba wapenzi wa mchezo wa ngumi kujitokeza kwa wingi kupata burudani kutoka kwa mabondia wa kike na kiume kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara pamoja na wengine kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama Tanzania.

Natanguliza shukrani na kuomba ushirikiano wa kutangaza mashindano hata.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s