MAPAMBANO YA KUOKOA MTO RUHAA YAANZA 

​Mbeya. Kampuni ya Highland Estates inayolima mpunga wilayani Mbarali imepewa agizo la kusafisha mifereji yote inayozunguka shamba lao ili kuruhusu maji kupita kwa urahisi kwenda mto Ruaha.

Agizo hilo limetolewa na kikosi kazi cha kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha kilichoko mkoa wa Mbeya.

Pia wametakiwa kuanza taratibu za kupatiwa cheti cha ukaguzi wa athari za mazingira kitoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho, Richard Muyungi alisema uongozi wa shamba hilo wafanye juhudi za ziada kutunza mazingira yote yanayozunguka shamba hilo na kuhakikisha maji yanapita kwa urahisi katika mifereji ya matoleo ya kupeleka maji mto Ruaha Mkuu.

“Tunawapa mwezi mmoja  mfanye ukarabati na mrekebishe hali ya usafi katika mifereji  ya shamba lenu baada ya muda huo tutarudi kwa ajili ya kukagua.” amesema Muyungi

Kikosi kazi hiko pia kilitembelea katika shamba la Kapunga Rice Project na kujionea matumizi mabaya ya maji kwa  kuyachepusha bila vibali  kunakofanywa na wananchi walio maeneo ya jirani.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s