MKUTANO WA KAFU WAVAMIWA NA WATU WASIO JULIKANA 

Watu wasiojulikana wakiwa na bastola wamevamia mkutano wa wanachama wa CUF ambao wanamuunga mkono, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad na kuwapiga wanachama wa CUF pamoja na waandishi wa habari ambao walikuwepo eneo hilo. 

            Maalim Seif Shariff Hamad
Mkutano huo ambao ulikuwa na lengo la kumtambulisha Katibu Mkuu wa CUF, inadaiwa watu hao waliovamia mkutano huo na kufanya vurugu ni wanachama wa Cuf ambao wanamuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba.
Kwa mujibu wa taarifa zilizokuwepo mkutano huo ulipangwa kufanyika majira ya saa tano za asubuhi katika hoteli ya Vina, Mabibo lakini kabla ya kuanza waliibuka watu hao wasiojulikana wakiwa wamevalia soksi nyeusi usoni kuficha sura zao na kususha kipigo kwa baadhi ya wanachama wa CUF waliokuwepo katika eneo hilo na waandishi wa habari. 

Mtu mmoja ambaye bado hajafahamika jina lake miongoni mwa waliovamia mkutano wa wanachama wa CUF ameshambuliwa na wananchi wakati akijaribu kutoroka.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s